Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini wilayani Chato mkoani Geita tarehe 11 Oktoba, 2018.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Chabulongo wilayani Chato.

Pamoja na kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini, alizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Ilyamchele, Njia panda ya Katende na Chabulongo.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akilakiwa na wananchi katika Kijiji cha Njiapanda ya Katende wilayani Chato kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho.

Aidha alizindua huduma ya umeme katika Shule ya Sekondari ya Emau iliyo katika Kijiji cha Kahumo.

Dkt Kalemani pia alitembelea kijiji cha Kikumbaitale ambapo aliagiza kuwa Kijiji hicho kiwekewe umeme ifikapo tarehe 20 mwezi huu.

Katika ziara hiyo Dkt Kalemani aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Mtemi Msafiri Semeon,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato,   Eliud Mwaiteleke watendaji wa Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Na Teresia Mhagama