Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 10 Agosti, 2018 amezidua rasmi mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kusambaza Gesi Asilia       majumbani mkoani     Mtwara.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kushoto) mara bada ya kuzidua mradi wa ujenzi wa mtambo wa usambazaji wa gesi asilia majumbani mkoani Mtwara. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakiwa pamoja na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (wa tatu kulia) na wa kwanza kulia Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota.

Waziri Kalemani, amefanya zoezi hilo leo katika shule ya Ufundi ya Mtwara mara baada ya kuzidua MW4 za umeme katika kituo cha Umeme       cha Mtwara.

Waziri Kalemani alisema kuwa, ujenzi wa mtambo huu umegharimu jumla ya billioni 1.5 kwa ajili ya kuwapelekea watumiaji wa awali wasiopungua 150 ambao bada ya miezi mitatu wataanza       kutumia   gesi  hiyo  majumbani.

Aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia ni madogo sana yaani ni kama hayapo, kwa kuwa wananchi wengi wanatumia kuni na mkaa kwa    wengi        kuliko       gesi.

“Sasa mtugi wa gesi ni takriban shilingi 55,000/- lakini ukitumia gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani itakuwa shilingi 25,000/- na utatumia kwa mwezi mzima hivyo ni nafuu kwa mwananchi wa Tanzania,” alisema     Wazari         Kalemani.

Mwezi mei tulianza matumizi ya gesi manyumbani lakini leo tumeanza matumiz ya gesi asilia katika mkoa wa Mtwara.

“hayawi hayawi yamekuwa,” alisema Waziri Kalemani.

Aidha, Waziri Kalemani aliendelea kueleza kuwa, Kuna magari zaidi ya 100 wanatumia gesi asilia jijini Dar es Salaam, hivyo kuazia mwezi Machi mwaka kesho (2019) tutaanza usanifu ili magari ya mkoa wa Mtwara nayo yaanze kutumia gesi asilia.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa, anawakaribisha wananchi wa Mtwara na Lindi kuwekeza zaidi kwenye shughuli za uchumi kwa kuwa masuala ya viwanda yanahitaji umeme na matumizi ya kawaida yanahitaji umeme na nimatumaini yake kuwa wananchi watatumia fursa hii vizuri.

Waziri Kalemani pia alitoa wito kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanza kutoa elimu mara moja kwa wiki kwa Chuo cha Ufundi cha Mtwara ili kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo wanapata uelewa mzuri katika matumizi ya gesi     asilia kwa  matumizi  ya nyumbani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amempongeza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kuwa sasa wananchi wa Mtwara wataanza  kunufaika         na gesi asilia.
Mkuu wa Mkoa Byakanwa alieleza kuwa,  umeme tunaoutumia kwa sasa, asilimia 60 inatokana na gesi asilia na sasa gesi hii inaweza kutumika kwa matumizi ya majumbani na wananchi watanufaika moja kwa moja na gesi asilia inayozalishwa kutoka Mkoa       wa    Mtwara.

Akizungumza katika uziduzi huo alisema kuwa, sasa wananchi wa Mtwara watafaida kwa kutumia gesi hii kwa bei nafuu, na faida nyingine ni kuhifadhi mazingira yetu vizuri maana tutaepukana na ukatajiwa      miti.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali serikalini pamoja na wabunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (mwenye kilemba) na wa nne kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota.

Kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Mkoa Byakanwa alitoa wito kwa wananchi kuweka mazingira wezisha ya kupata gesi majumbani kwetu.

“Tuboreshe miundombinu ili tupata gesi kwa urahisi, lakini pia tuwe na nyumba zinazokidhi viegezo ili usambazaji wa gesi asilia ufike kwa urahisi majumbani kwetu,” alisema Byakanwa.

Akizungumza katika uziduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Byakanwa aliwaambia wanafunzi wa Shule ya Ufundi ya Mtwara kuwa Serikali imehakikisha kuwa shule hii inakuwa kati ya taasisi ambayo itafaidika na matumizi ya gesi asilia.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alimpongeza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard kalemani kwa kuwa msikivu na mwepesi wa kutimiza ahadi zake kwa wabunge wezake.

Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alitoa wito kwa TPDC kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwa wananchi wa Mtwara na Lindi ili kuondoa uoga kwa wananchi na kuwaelimisha matumizi bora ya gesi asilia na hivyo kufaidika na gesi hiyo ipasavyo.

Na Rhoda James – Mtwara