A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2017/18 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake kwa Mwaka 2018/19.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kutekeleza majukumu yangu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu. Vilevile, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutekeleza kazi zao za Kibunge na kushiriki Mkutano huu wa 11 wa Bunge lako Tukufu.

3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nitumie fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo makini wanayonipatia ili kuhakikisha kuwa azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda inafikiwa. Ni wazi kuwa viongozi wetu hawa wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa maelekezo yenye lengo la kuhakikisha kuwa umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wa gharama nafuu unazalishwa ili kuchochea ukuaji wa viwanda hapa nchini. Nampongeza Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuiongoza vyema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Read more….