Tarehe 12 Aprili, 2018 Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja na kutatua changamoto mbalimbali.

Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (kushoto) akielezea kazi za mita za kupimia mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kulia)

Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Kamishna Luoga alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.