Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua mwishoni mwa wiki tarehe 06 Aprili, 2018 alikutana na wadau wa maendeleo katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili miradi ya umeme nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (hayupo pichani) katika kikao hicho

Wadau wa maendeleo walioshiriki katika kikao hicho walitoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (WB) Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP). Wengine walioshiriki ni pamoja na wawakilishi kutoka balozi zilizopo nchini za Marekani, Norway, Sweden na wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na la Maendeleo la Tanzania (TPDC).

Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani)