Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, tarehe 30 Septemba, 2018  amewasha umeme katika Kijiji cha Msunjulile B kilichopo katika Kata Sejile wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika Kijiji cha Msunjulile B wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi.

Kuwashwa kwa  umeme katika Kijiji hicho kunafanya Vijiji vyote Sita katika Kata hiyo ya Sejile kupata huduma ya umeme.

Dkt Kalemani amempongeza mkandarasi anayesambaza umeme katika Wilaya hiyo, kampuni ya A2Z pamoja na Meneja wa Tanesco wa Wilaya ya Kongwa kwa kazi nzuri wanayofanya  ya kusambaza umeme. Hata hivyo aliagiza kuwa kazi ya kusambazia umeme wananchi wengine iendelee.

Akiwa kijijini hapo, Dkt  Kalemani aligawa kwa wananchi vifaa 20  vya Umeme Tayari (UMETA) ambapo wananchi hao wataunganishiwa umeme bila kuingia gharama ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msunjulile B wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma.