Wananchi katika kijiji cha Rutunguru wilayani Chato tarehe 31 Machi, 2018 wameanza kupata huduma ya umeme baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani.

Kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu (REA III) ambapo kaya 52 zinatarajiwa kuunganishiwa nishati hiyo.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rutunguru mara baada ya kuwasha umeme katika Shule ya Msingi Rutunguru.

Kabla ya uzinduzi huo, Waziri wa Nishati aliwapongeza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa jitihada zilizopelekea umeme kufika kijijini hapo.

Wananchi mbalimbali katika kijiji hicho, waliishukuru Serikali kwa kufikishiwa huduma ya umeme na kueleza kuwa nishati hiyo itawasaidia katika kufanya shughuli mbalimbali hasa za kiuchumi.

Na Mwandishi wetu, Chato.