Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini, (REA) imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme vijiji awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza na kusema kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (katikati), akizungumza wakati wa katika kikao chake na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati vijijini (REA) wakati alipokutana na bodi hiyo, Juni 17, 2020,Jijini Dodoma,kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Zena Said.

Mwenyekiti wa bodi hiyo , Wakili Julias Kalolo, hiyo ilimueleza  Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani, wakati alipokutana na bodi hiyo, Juni 17, 2020,Jijini Dodoma,ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa REA awamu ya Tatu mzunguko wa pili unaotajaria kuanza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa REA III mzunguko wa kwanza utakaokamilika Juni 30,2020.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine, Dkt. Kalemani alidhirishwa na hatua zilizofikiwa juu ya utekelezaji wa REA III mzunguko wa kwanza na kusema kuwa anaimani mradi huo utakamilika kama ulivyopangwa hivyo aliitaka bodi hiyo kuendelea kufanya kazi yake kwa weledi kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Vilevile aliipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri waliofanya, pia aliitaka kuendelea kutoa ushauri juu ya miradi inayoendelea.

Aidha Dkt. Kalemani aliieleza kuwa mikutano ya namna hiyo ni ni muhimu katika kuboresha utekelezaji wa miradi inayoendelea ili kuondokana na changamoto zilizojitokeza katika miradi iliyotanguali.

ZUENA MSUYA-DODOMA