Dibaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 07 Oktoba, 2017 alibadilisha Majukumu ya iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kwakuanzisha Wizara ya Nishati kupitia Tamko Namba 144 la 2016. Wizara hii ilipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sera za Nishati, Mafuta na Gesi, Usimamizi wa Rasilimali za Nishati, Petroli, Ununuzi wa Mafuta kwa Pamoja, Maendeleo ya Nishati Vijijni na Mijini na Nishati Mbadala; kusimamia ufanisi katika maendeleo ya Rasilimali watu pamoja na Taasisi na Idara zilizo chini yaWizara na Miradi iliyochini ya Wizara.