Huduma za Kisheria

Lengo

Kutoa utaalam na huduma za kisheria kwa wizara.

Majukumu

(i)       Kutoa ushauri wa kisheria katika nyanja ya Nishati;

(ii)      Kuandaa rasimu na nyaraka za kisheria, na vyombo vya sharia zinazohusu sekta ya nishati na kuziwasilisha kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa ukaguzi na makamilisho;

(iii)     Kutoa msaaada wa kitaalamu kwa AGC juu ya  ya vyombo vya kisheria vinvyopitia  rasilimali za sekta ya  nishati;

(iv)     Kuandaa  na kutoa mchango katika majadiliano ya mikataba ya wizara;

(v)      Kutoa mchango na kusaidia katika usuluhishi na uamuzi wa migogoro inayohusu wizara;

(vi)     Kuwa msimamizi  wa mikataba yote iliyopo katika wizara na kutoa ushauri wa usimamizi wa mikataba hiyo kwa kushirikiana na mwanasheria mkuu;

(vii)    Kushirikiana na AGC juu ya madai ya kesi za umma na madai mengine yanayohusisha wizara.

(viii)   Kutoa ushauri wa kisheria na msaada kwa mambo yote ya utawala, fedha, na manunuzi kwa kushirikiana na ACG.

Sehemu hii itakuwa chini ya Mkurugenzi.