Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara

Q: Wizara ya Nishati ilianzishwa lini?

A: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 07 Oktoba, 2017 alibadilisha Majukumu ya iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kwakuanzisha Wizara ya Nishati kupitia Tamko Namba 144 la 2016.

Q: Wizara ya Nishati ina majukumu gani?

A: Wizara hii ilipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sera za Nishati, Mafuta na Gesi, Usimamizi wa Rasilimali za Nishati, Petroli, Ununuzi wa Mafuta kwa Pamoja, Maendeleo ya Nishati Vijijni na Mijini na Nishati Mbadala; kusimamia ufanisi katika maendeleo ya Rasilimali watu pamoja na Taasisi na Idara zilizo chini yaWizara na Miradi iliyochini ya Wizara .

Q: Nini dira na dhamira ya Wizara ya Nishati?

A: Dira Kuhamasisha, kuwezesha na kusimamia maendeleo na matumizi endelevu ya rasimali za Nishati kwa manufaa ya Watanzania.

Dhima Kuwa Taasisi yenye ufanisi itakayo hakikisha kuwa rasilimali za Nishati zinachangia ipasavyo katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya Wananchi wa Tanzania.