Mawasiliano Serikalini

Lengo

Kutoa utaalam na huduma katika taarifa, mawasiliano na mijadala ya wizara  kwa umma na kwa vyombo vya habari.

Majukumu ya kitengo: –

(i)       Kutoa na kusambaza nyaraka kama vipeperushi, Makala, majarida nk ili kuufahamisha umma juu ya sera, programu, shughuli a mabadiliko yanayotokea ndani ya wizara;

(ii)      Kuratibu mikutano ya vyombo vyna wizara;

(iii)     Kushiriki katika mijadala na umma na vyombo vya habari kwa mambo yanayohusiana na wizara;

(iv)     Kutangaza shughuli, programu, na sera za wizara;

(v)      Kuratibu maandalizi ya nyaraka, za  kisekta na kiwizara kwa ajili ya warsha  na mikutano;

(vi)     Kuratibu maandalizi na utoaji wa Makala na magazeti ya wizara;

(vii)    Kuelimisha umma juu ya  uwekezaji katika sekta ya nishati na madini;

(viii)   Kuboresha taarifa za kisekta na za kiwizara katika tovuti

(ix)     Kushauri vitengo, na sehemu, taasisi za ummazisizo za kibiashara juu ya utoaji wa nyaraka mbalimbali.

Sehemu hii itakuwa chini ya Afisa habari mkuu.