Mazingira

Lengo

Kuhakikisha uvumbuzi , utafutaji, na uzalishaji wa nishati vinakuwa rafiki wa mazingira.

Sehemu hii itakuwa na amajukumu yafuatayo:-

(i)       Kuhakikisha Mpango wa Usimamizi wa mazingira katika wizara unafwatwa;

(ii)      Kuchochea ukaguzi wa mazingira ili kutathmini utendaji wa shughuli za sekta ya nishati na kubaini maeneo yanayohitaji marekebisho;

(iii)     Kutoa ushauri juu ya sera, na mapitio ya kisheria katika usimamizi wa mazingira katika sekta ya nishati kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira;

(iv)     Kufunga, kusimamia, kutunza, na kuhakikisha kanzi data ya usimamizi wa mazingira inafanya kazi ;

(v)      Kusimamia utunzanji wa mazingira katika miradi ya utafutaji wa gesi na mafuta;

(vi)     Kusimamia ulinzi wa mazingira katika kuhifadhi na kusafirisha petrol na gesi;

(vii)    Kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kupunguza athari za kijamii na kiuchumi  zitokanazo na shughuli za uvumbuzi na utafutaji wa gesi na mafuta.

(viii)   Kuandaa  ukaguzi wa mazingira ya sekta ya nishati kwa kuangalia sharia, kanuni, sera, mipango, mikakati na programu.

Kitengo hiki kitakuwa chini ya Afisa mkuu wa fani husika.