Petroli na Gesi

Lengo

Kusimamia Kusimamia utafutaji  endelevu wa petroli, na kuendeleza rasilimali za  Petroli na gesi asilia nchini.

Majukumu

(i)       Kukuza sera, mipango na programu zinazohusiana na  Petroli na rasilimali za gesi asilia ili kuhakikisha ufanisi, gharama nafuu, udhabiti na huduma bora katika mazingira rafiki;

(ii)      Kukuza maendeleo endelevu na utafutaji  wa rasilimali za petroli;

(iii)     Kutathmini na kuchanganua adhari zitokanazo na ajali au majanga yatokanayo na shughuli za Petroli kwa kushirikiana na mamlaka husika;

(iv)     Kuvutia uwekezaji wa nje na teknolojia katika sekta ya Petroli;

(v)      Kukuza ushiriki wa ndani katika sekta ya Petroli;

(vi)     Kuratibu maendeleo ya miundombinu ya petroli na gesi asilia kwa ajili ya usambazaji salama;

(vii)    Kusimamia utoaji, ufufuaji, uhairishaji na ufutaji  wa leseni za utafutaji na maendeleo ya Petroli.

(viii)   Kufanya tafiti na kuchunguza rasilimali za  petroli na kukuza ufanisi na matumizi endelevu ya rasilimali za petroli.

Kitengo hiki kitaongozwa na Kamishna na kitakuwa na sehemu kuu tatu (3):

(i)       Petroli;a

(ii)      Gesi Asilia;

(iii)     Maendeleo ya Petroli .

Petroli

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:-

(i)       Kutengeneza  Mipango na programu kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya Petroli yenye ufanisi, gharama nafuu, madhubuti, na huduma bora katika mazingira rafiki;

(ii)      Kufanya tafiti zinazohusiana na petroli, na kutoa ushauri juu ya matumizi ya teknolojia sahihi na njia za lazima zitakazo pelekea ufanisi wa sekta ya petrol.

(iii)     Kuratibu shughuli za ngazi za juu na  za chini katika ngazi ya taifa na ya mkoa kwa lengo la kukuza msingi wa  rasilimali za nishati na usambazaji madhubuti wa bidhaa za petroli na gesi asilia;

(iv)     Kuweka mfumo madhubuti ili kuwa na  ufanisi katika manunuzi na matumizi ya bidhaa za vimiminika vya petroli nchini; kusimamia na kutoa tathmini;

(v)      Facilitate value addition and value chain development in the petroleum industry;

(vi)     Prepare and implement emergency supply plan in case of disruption of supply in the country;

(vii)    To promote local participation in the petroleum industry; and

(viii)   Raise public awareness on petroleum activities and develop strategies to promote local participation and international cooperation.

Sehemu hii itakuwa chini ya kamishna msaidizi.

Gesi Asilia

Majukumu ya sehemu hii ni kama yafuatayo:-

(i)       Kutoa ushauri juu ya sera muafaka na miongozo inayohitajika kwa ajili ya matumizi sahihi ya rasilimali za gesi asilia;

(ii)      Kushauri juu ya taasisi  zilizoko katika sekta hizo, zinazokidhi vigezo katika kutoa huduma bora za gesi asilia;

(iii)     Kufwatilia na kutathmini utendaji wa sekta ya gesi asilia ikiwa ni pamoja na uhifadhi, usafirishaji, usambazaji na masoko,

(iv)     Kukuza uwekezaji wa miradi inayotumia gesi asilia;

(v)      Kuratibu mabadiliko ya ongezeko la thamani , na mzunguko wa thamani katika sekta ya petroli.

(vi)     Kufanya tafiti juu ya uwezo wa ndani katika kutoa bidhaa na huduma zinazohitajika katika sekta ya petroli na kutoa mapendekezo ya njia za kuboresha uwezo wa ndani;

(vii)    Kukuza ushiriki wa ndani katika sekta ya petroli.

(viii)   Kukagua uanzishwaji wa miradi ya gesi asilia na kusimamia mikataba.

Sehemu hii itakuwa chini ya Kamishna msaidizi.

Maendeleo ya Petroli.

Sehemu hii itakuwa na amjukumu yafuatayo:-

(i)       Kutengeneza, kusimamia, kutathmini utekelezaji na kupitia sera na vyombo vya sera kwa kanuni sahihi na usimamizi wa maendeleo ya petroli;

(ii)      Kutengeneza Mpango mkuu wa matumizi ya gesi ili kupata mwongozo wa matumizi sahihi ya gesi asilia na kuongeza  uwekezaji kwa miradi inayotumia gesi asilia.;

(iii)     Kufanya chunguzi wa mambo yanayohusiana na mendeleo ya gesi asilia.;

(iv)     Kuweka mpango mkakati ilikuimarisha utendaji wa sekta ndogo ya Petroli.;

(v)      Kuratibu mapitio ya taratibu za kitaasisi za sekta ndogo ya Petroli ili kukuza ushirikiano katika kuandaa na kutekeleza sera ya taifa inayohusu petroli.;

(vi)     Kutmbua mapungufu na kupendekeza hatua stahiki ili kuboresha usambazaji wa nishati, uwepo wa nishati, udhabiti, na upatikanaji kwa gharama nafuu ili kuboresha utendaji wa sekta ndogo ya petroli;

 (vii)   Kufanya tafiti juu ya  rasilimali za petrol na kutoa mwelekeo wa  kutoa maamuzi ya wazi kwa ajili ya mwenendo wa baadae wa sekta ndogo ya petroli;

(viii)   Kukuza na kuwezesha ushiriki wa taasisi binafsi katika sekta ya petroli kupitia sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) na kuboresha muundo wa udhibiti katika kukuza uwekezaji wa haraka wa miradi ya petrol;

(ix)     Kuandaa na kuboresha kanzidata ya taarifa za nishati ya petroli na kutoa matangazo na takwimu kuhusiana na nishati ya petroli;

(x)      Kukusanya, kuchunguza na kuchanganua takwimu zinazohitajika katika uundwaji na utekelezaji wa sera, mipango na makisio ya bajeti..

Sehemu hii itakuwa chini ya Kamishna msaidizi.