Sera na Mipango

Lengo

Kutoa huduma za kitaalamu katika uundwaji wa sera, utekelezaji, ufwatiliaji na tathmini.

Majukumu

(i)       Kuratibu maandalizi ya sera za kiwizara, na kufuatilia utekelezaji wake na pia kufanya tathmini ya athari zake;

(ii)      Kuchanganua sera kutoka katika sekta zingine na kutoa ushauri ipasavyo;

(iii)     Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti za wizara;

(iv)     Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango na bajeti za wizara na kuandaa ripoti za utendaji;

(v)      Kufanya tafiti, ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya wizara na kutoa misingi kwa ajili ya kufanya maamuzi kwa ajili ya muelekeo wa  baadae wa wizara;

(vi)     Kusimamia mikataba ya utendaji.

(vii)    Kuhimiza na kuwezesha sekta binafsi kutoa  huduma katika wizara;

(viii)   Kuratibu maandalizi ya michango ya wizara katika hotuba za bajeti na pia katika ripoti ya mwaka ya uchumi.;

(ix)     Kurasimisha mpango mkakati, bajeti na njia za ufuatiliaji na tathmini katika wizara;

(x)      Kuwa msimamizi na mratibu wa takwimu za kiwizara.

(xi)     Kuhakikisha mipango ya kiwizara na bajeti vinaingizwa katika mchakato wa bajeti ya serikali.

Kitengo hiki kitakuwa chini ya Mkurugenzi na kitakuwa na sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:-

(i)       Sera na Mipango

(ii)      Ufwatiliaji na tathmini.(Monitoring and Evaluation)

Sera na mipango

Sehemu hii itakuwa na majukumu  yafuatayo:-

(i)       Kuratibu muundo, mapitio, utekelezaji na ufwatiliaji wa sera za wizara; na kuhakikisha ziko sawia na sera za Taifa , miundo na mikakati.;

(ii)      Kupitia na kutoa ushauri juu ya matoleo ya sera yanayoandaliwa na wizara.

(iii)     Kufanya tafiti na uchunguzi wa athari za sera za wizara na kutoa mwongozo wa kufanya maamuzi ya kina kwa mwelekeo wa baadae wa wizara;

(iv)     Kukusanya ripoti za utekelezaji za ilani ya chama tawala na ripoti za kamati za bunge;

(v)      Kuratibu uundwaji na maandalizi ya mpango mkakati wa mhula wa kati wa wizara, mpango wa utekelezaji wa mwaka, na bajeti;

(vi)     Kukusanya ripoti za miradi ya kiwizara, programu na mipango ya utekelezaji na kutengeneza mbinu za upatikanaji wa rasilimali;

(vii)    Kuwasiliana na wizara ya Feddha na mipango, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma juu ya Mpango mkakati na mchakato wa bajeti;

(viii)   Kutoa mwongozo wa kitaalamu na msaada katika kurasimisha Mpango mkakati na mchakato wa bajeti katika wizara;

(ix)     Kuandaa mkataba wa maridhiano kwa miradi na program zenye ufadhili wa kimataifa;

(x)      Kuratibu na kuandaa hotuba ya bajeti ya wizara.

(xi)     Kushiriki katika uchambuzi wa kutafuta huduma za kutoka nje (Ushiriki wa sekta binafsi)  

Sehemu hii itakuwa chini ya mkurugenzi msaidizi.

3.4.2 Ufwatiliaji na Tathmini

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:-

(i)       Kufwatilia na kutathmini utekelezaji wa Mpango wa wizara wa  mwaka na mpango mkakati wa kati;

(ii)      KuandaaRipoti za utendaji za mara kwa mara;

(iii)     Kukusanya, kuchunguza, na kuchanganua takwimu zitakazotumika katika muundo na utekelezaji wa sera, mipango na makisio ya bajeti;

(iv)     Kutoa mchango katika maandalizi ya mipango, programu, na shughuli za bajeti ndani ya wizara ikiwa ni pamoja na kuweka na kuweka malengo ya utendaji kazi na viashiria;

(v)      Kutoa ushauri  wa kitaalam ikiwa ni pamoja na urasimishaji wa mchakato wa ufwatiliaji na tathmini.

(vi)     Kufanya tafiti na tathmini ya mipango, miradi na programu zinazoendeshwa na wizara;

(vii)    Kusimamia mikataba ya kiutendaji;

(viii)   Kukusanya taarifa za  utoaji huduma, kukusanya maoni ya wadau/wateja/na kushauri uongozi ipasavyo;

(ix)     Kuratibu mapitio ya utendaji ya kati ya mwaka na mwisho wa mwaka.;

(x)      Kuratibu ukusanyaji, uchambuzi, tafsiri na uwasilishaji wa taarifa na takwimu za wizara;

(xi)     Kuwa msimamizi na kitovu cha takwimu za wizara;

(xii)    Kusimamia utendaji wa taasisi zilizoko chini ya wizara.

Sehemu hii itakuwa chini ya Mkurugenzi msaidizi.