Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Lengo

Kutoa utaalamu na huduma juu ya matumizi ya TEHAMA katika wizara.

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:-

(i)       Utekelezaji wa sera ya TEHAMA na ile ya Serikali mtandao;

(ii)      Kutengeneza na kuratibu Mfumo akisi wa TEHAMA katika wizara;

(iii)     Kuhakikisha vifaa na programu za kompyuta zinatunzwa vizuri;

(iv)     Kuratibuu na kutoa ushauri katika manunuzi ya programu na vifaa vya wizara;

(v)      Kuunda na kuratibu matumizi ya barua pepe katika mfumo wa ndani na wa nje ya wizara.

(vi)     Kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo ya maeneo yatakayotumia TEHAMA kama chombo kitakachoboresha utoaji wa huduma kwa wizara nzima.

Sehemu hii itakuwa chini ya Afisa TEHAMA mkuu.