Uhasibu na Fedha

Lengo

Kutoa huduma ya usimamizi wa fedha na utunzaji wa vitabu vya fedha kwa wizara.

Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-

Mishahara

(i)       Kuandaa malipo ya mishahara pamoja na makato yaliyowekwa kisheria;

(ii)      Kuandaa nyaraka za pensheni

(iii)     Kutunza kumbukumbu za mishahara.

Ofisi ya Malipo

(i)       Kutuma orodha ya vocha za malipo kwa wizara;

(ii)      Kukusanya hundi zote kutoka hazina;

(iii)     Kupeleka benki fedha taslim na hundi;

(iv)     Kuandaa muhtasari wa ripoti ya mwezi;

(v)      Kuwalipa waanyakazi, watoa huduma kwa fedha taskim na kwa hundi

(vi)     Kupanga vocha zilizolipwa;

(vii)    Kutunza kitabu cha fedha taslim;

(viii)   Kuweka kumbukumbu ya masurufu yaliyotolewa.

(ix)     Kuandaa na kufanya malipo yote.

Mapato

(i)       Kukusanya mapato yote;

(ii)      Kusimamia mapato kulingana na kanuni na miongozo;

(iii)     Kukusanya kodi ya mwaka, ada ya maombi ya leseni za madini, hakimiliki, na kodi nyinginezo.

(iv)     Maridhiano ya benki.

Pensheni

(i)       Kuandaa malipo ya pensheni

(ii)      Kutunza kumbukumbu za pensheni.

Bajeti

(i)       Kusimamia mgao na matumizi;

(ii)      Kuandaa hesabu za mwisho na taarifa nyinginezo za fedha..

Ukaguzi wa awali (Examination:)

(i)       Kuchunguza nyaraka zote zinazoambatana na vocha,  pamoja na kuidhinisha kulingana na taratibuku;

(ii)      Kufanya ukaguzi wa awali ili kuhakikisha sheria, kanuni na waraka zote zimefwatwa.

(iii)     Kujibu maswali yote ya ukaguzi yaliyojitokeza katika mwaka wa fedha uliopita.

Sehemu hii itakuwa chini ya mhasibu mkuu.