Ukaguzi wa Ndani

Lengo

Kutoa huduma za ushauri kwa Mkuu wa uhasibu juu ya usimamizi sahihi wa rasilimali.

Majukumu ya sehemu ya ukaguzi wa ndani:-

(i)       Kupitia ripoti ya udhibiti sahihi juu ya kupokea, kutunza, na matumizi ya rasilimali zote za wizara;

(ii)      Kupitia na kuripoti taratibu zote za fedha na za kiutendaji zilizowekwa na mamlaka ya kisheria au maelekezo ili kudhibiti matumizi ya wizara kwa ulinganifu;

(iii)     Kupitia na kuripoti juu ya mipangilio  sahihi ya mgao katika akaunti za mapato na matumizi;

(iv)     Kuunda taratibu za zitakazowezesha kuendana na viwngo vya kimataifa kila mwaka;

(v)      Kupitia na kuripoti juu ya uthabiti na uadilifu katika taarifa za fedha na uendeshaji na kuandaa taarifa za fedha na ripoti nyinginezo;

(vi)     Kupitia na kuripoti mfumo uliopo wa kutunza mali na kuthibitisha uwepo wa mali hizo;

(vii)    Kupitia na kuripoti juu ya shughuli au programu ili kuhakikisha kama matokeo yanaendana na nia na malengo yaliyowekwa.

(viii)   Kupitia na kuripoti muitikio wa uongozi wa juu kwa taarifa za ukaguzi wa ndani, na kuusaidia uongozi katika kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na taarifa za ukaguzi, na kufwatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali;

(ix)     Kupitia na kuripoti juu ya utoshelevu wa vidhibiti vilivyowekwa  katika mifumo ya kompyuta;

(x)      Kuandaa na kutekeleza Mipango mkakati ya ukaguzi

(xi)     Kufanya ukaguzi wa utendaji katika kutathmini miradi ya maendeleo.

Sehemu hii itakuwa chini ya mkaguzi mkuu wa ndani.