Ununuzi na Ugavi

Lengo

Kutoa utaalam na huduma katika manunuzi, uhifadhi na ugavi wa bidhaa na huduma katika wizara.

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:-

(i)       Kushauri Uongozi kwenye masuala ya nayohusiana na manunuzi ya bidhaa na huduma pamoja na kusimamia usafirishaji;

(ii)      Kusimamia taratibu zote za manunuzi kufuatana na sharia ya manunuzi ya umma;

(iii)     Kuandaa Mpango wa mwaka wa manunuzi ya wizara;

(iv)     Kununua, kutunza, na kusimamia bidhaa, vifaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya ugavi katika wizara;

(v)      Kutunza na kusimamia usambazaji wa vifaa vya ofisi na vitendea kazi;

(vi)     Kutunza na kuboresha orodha ya bidhaana vifaa;

(vii)    Kutoa huduma ya sekretariet kwenye bodi ya zabuni ya wizara kulingana na sharia ya manunuzi ya umma;

(viii)   Kuweka viwango vya bidhaa na huduma zilizonunuliwa na kuhakikisha thamani yake inaendana na thamani ya fedha iliyotumika.

(ix)     Kuandaa mpango wa utekelezaji, ripoti ya maendeleo na bajeti kwa kitengo cha manunuzi.

Kitengo hiki kitakuwa chini ya mkurugenzi.