Utawala na Rasilimali watu

Lengo

Kutoa utaalamu na huduma za usimamizi wa  rasilimali watu na mambo ya utawala katika wizara.

Majukumu

(i)       Kutoa ushauri juu ya mambo yanayohusu utawala na rasilimali watu.;

(ii)      Kutoa mchango katika mambo yanayohusu utawala na rasilimali watu ikiwa ni  pamoja na kuajiri, maendeleo ya rasilimali watu na mafunzo, kupandisha vyeo, maadili, kuwafanya watumishi kubaki katika taasisi bila kuhama (retention), motisha, utendaji na maslahi ya wafanyakazi.;

(iii)     Kuhakikisha ubora wa hali ya juu, na ufanisi katika  usimamizi na matumizi ya rasilimali watu ndani ya Wizara;

(iv)     Kuwa kiungo kati ya wizara na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma katika utekelezaji wa Usimamizi wa utumishi wa umma, sera ya ajira, na Sheria husika za Utumishi;

(v)      Kusimamia maslahi ya wafanyakazi.

Kitengo hiki kitakuwa chini ya Mkurugenzi na kitakuwa na sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:-

(i)       Sehemu ya Utawala;

(ii)      Sehemu ya Rasilimali watu.

Sehemu ya Utawala

Majukumu ya sehemu hii ni kamayafuatayo: –

(i)       Kutafsiri na kuhakikisha utekelezwaji wa taratibu za utumishi wa umma, kanuni za kudumu za utumishi wa umma (standing orders), na sheria za kazi;

(ii)      Kuwezesha maswala na maslahi ya mfanyakazi ikiwa ni pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;

(iii)     Kutoa huduma ya masijala, tarishi, na kutunza nyaraka za ofisi;

(iv)     Kusimamia maswala ya itifaki;

(v)      Kuhakikisha uwepo wa  huduma za ulinzi, usafiri, na matumizi mengine kwa ujumla;

(vi)     Kuhakikisha matengenezo ya vifaa, majengo na maeneo ya ofisi;

(vii)    Kuratibu utekelezaji wa maadili na kanuni;

(viii)   Kutekeleza mambo mbalimbali.

(ix)     Kuratibu utekelezwaji wa ushiriki wa sekta binafsi, maendeleo ya kibiashara na mkataba wa huduma kwa wateja.

(x)      Kuishauri wizara maswala yanayohusu ufanisi wa muundo.

Sehemu hii itakuwa chini ya Mkurugenzi msaidizi.

Sehemu ya Rasilimali watu

Majukumu ya sehemu hii ni kama yafuatayo:-

(i)       Kuratibu michakato ya ajira, usaili, kupanga nafasi, uhakiki, upandaji vyeo na uhamisho wa mfanyakazi;

(ii)      Kupanga mipango ya rasilimali watu ili kubaini uwepo na mahitaji ya wataalamu chini ya wizara, na kuwezesha utekelezaji wa mpango wa kurithishana madaraka (succession plan);

(iii)     Kuandaa Makisio ya mwaka ya mafao, na kusimamia mishahara na mfumo wa mishahara (payroll)

(iv)     Kuratibu utekelezaji wa mfumo wa mapitio ya  wazi ya utendaji na tathmini (OPRAS), kupima matokeo ya tathmini,; kuandaa taarifa za utekelezaji; na kufwatilia utekelezaji wa mapendekezo katika kila form ya mapitio ya wazi ya utendaji na tathmini;

(v)      Kuandaa na kuhifadhi  nyaraka za kutokuwepo kazini;

(vi)     Kusimamia mafao ya watumishi (pensheni, posho n.k) pamoj na stahili zao;

(vii)    Kuwezesha Mafunzo ya rasilimali watu ya wizara na kuongeza ujuzi;

(viii)   Kufwatilia na kutoa tathmini ya utekelezaji wa mafunzo, na kuandaa taarifa za mafunzo;

(ix)     Kufanya ukaguzi wa mahitaji ya wataalamu kwa ajili ya taasisi, kuandaa na kutekeleza mpango wa kuendeleza wafanyakazi

(x)      Kutoa taarifa, ufafanuzi na ripoti fupi juu ya rasilimali watu na masuala ya mafunzo.

Sehemu hii itakuwa chini ya Mkurugenzi msaidizi.