Mawaziri wanaoshughulikia Miundombinu pamoja na Nishati kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 21 Februari mwaka huu, wameshiriki Warsha iliyokutanisha Wadau mbalimbali kutoka Sekta za Miundombinu na Nishati lengo likiwa ni kutathmini fursa za uwekezaji zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, Kirundi Kivenjinja ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Uganda akieleza jambo katika Warsha ya Baraza la Mawaziri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda.

Warsha hiyo ilihusisha majadiliano ambayo yalizipa fursa nchi wanachama na Sekretarieti ya Afrika Mashariki kuonesha miradi yote ya muhimu kwa wawekezaji na Washirika wa Maendeleo hivyo kuwezesha miradi hiyo kupata fedha na kuanza kutekelezwa.

Na Rhoda James, Kampala

Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Rwegasila (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,, Adolf Mkenda na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Dkt. Adelardus Kilangi. Wengine katika picha ni wajumbe waliohudhuria warsha hiyo nchini Uganda.

 

 

Wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni pamoja na Taasisi za Serikali, Mashirika binafsi, Benki za Maendeleo, Taasisi za Kitaifa za Maendeleo, Mashirika ya Biashara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Asasi za Kiraia.