Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 10 Agosti, 2018 ameagiza Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa, umeme katika Mikao ya Mtwara na Lindi haikatiki  mara kwa  mara.

Mkurugenzi wa kituo cha umeme Mtwara cha Shirika la umeme Tanzania (TANESCO), Abdallah Ikwasi akitoa maezo kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) wakati wa uziduzi wa MW 4 katika kituo cha Umeme Mtwara.

Waziri Kalemani ameeleza hayo wakati wa uzinduzi wa mitambo 2 ya kuzalisha umeme MW 4 na kusema kuwa, baada ya kufungwa kwa mitambo hiyo mipya katika kituo cha kuzalishsha umeme cha Mtwara na kunganishwa kwanye gridi ya Taifa, hali ya umeme katika   Mikoa       ya Lindi na Mtwara itaimarika.

“Mitambo hiyo ifanye kazi kwa ufanisi na sitarajii umeme kukatika mara kwa mara kwenye mikoa hiyo,” alisema Waziri Kalemani

Aliongeza kuwa, kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi sasa kuna jumla ya MW 22, na kusema kuwa matumizi ya juu kwa Mikoa hiyo ni takriban MW 16 kwa hiyo tuna ziada ya MW 6.

“Lakini ziada ni kwa sasa, hatutakiwi kubweteka kwa kuwa Mtwara na Lindi bado kuna ujenzi wa viwanda vingi hivyo tunatakiwa kuendelea kuongeza umeme mwingi zaidi,” Alisema Waziri Kalemani.

Akizungumza katika uzinduzi huo alisema kuwa, mwezi Novemba mwaka jana (2017) tulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme pamoja na kuwa tulikuwa na mitambo 9 lakini iliyokuwa ikifanya kazi  ilikuwa     sita   tu.

Aliongeza kuwa, anawapongeza wafanyakazi wa TANESCO kwa kufanya kazi kubwa na kwa ufanisi. Pia, Waziri Kalemani aliwapongeza wafanyakazi wa TANESCO kwa kufanya ukarabati wa mashine hizo tatu ambazo zilikuwa zimeharibika lakini sasa zinafanya kazi.

Waziri Kalemani katika uzinduzi huo aliahidi wananchi wa Mtwara na Lindi kuwa watapata mashine nyingine mbili ili wawe na jumla ya      MW  26.

Aidha, Waziri Kalemani alieleza kuwa wameanza programu ya kufanya matengenezo (maintenance) kwa mashine hizo kila baada ya miezi mitatu ili kuepuka uharibifu uliokuwa umejitokeza hapo nyuma.

Waziri Kalemani alisema kuwa, Wizara itaetaendelea kuzalisha umeme kwa bei nafuu na tutaendelea kupitia bei zetu kadri tunavyoendelea kuzalisha umeme ili wananchi wa hali ya chini wawe na uwezo wa kuunganishwa na nishati hiyo ya umeme.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota alisema kuwa, Ingawa kuna ziada ya umeme katika Mikoa ya Mtwara na Lindi, bado vijijini wanahitaji umeme japokuwa kuna ziada         ya     umeme     wa    MW  6.

“Tunaomba uendelee kupeleka umeme vijijini maana wananchi bado wana uhitaji wa nishati hiyo,” alisema Abudalla

Naye Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia alisema kuwa kwa sasa shughuli za uzalishaji zitaongezeka na alimshukuru Waziri Kalemani na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuondoa kero ya umeme katika mikoa ya Mtwara na Lindi na kusisitiza kuwa wananchi sasa wahakikishe kuwa wanauganisha umeme ili kufaidika       nao.

Muonekano wa mashine mbili mpya za MW 4 baada ya uziduzi wa mashine hizo katika kituo cha umeme cha Mtwara.

Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema kuwa hali ya umeme ilikuwa ni mbaya  miezi tisa aliyokuja Mtwara, alieleza kuwa aliongea na Waziri Kalemani akamuahidi kuwa ataleta mashine mbili na leo hii hali ya umeme ni nzuri na anampongeza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kwa   kutimiza   ahadi         yake.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Byakanwa Pia limpongeza Waziri Kalemani na Wizara kwa ujumla kwa kuwa, kuna baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa hayana umeme kabisa lakini sasa kuna umeme    kila   mahali.

“Nenda wilaya yoyote kama vile,  Nanyumbu, Newala, Masasi utakuta wana umeme kila mahali na haukatiki mara kwa mara kama hapo nyuma,” alisema Mkuu wa Mkoa Mtwara.

Halikadhalika, alitoa wito kwa wananchi kuwekeza kwenye Viwanda na pia kuhakikisha kuwa sasa wanauganisha umeme kwenye     nyumba    zao.

Na Rhoda  James – Mtwara