Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, leo, Juni 29, 2018 ameongoza kikao cha Uongozi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiongoza kikao cha Uongozi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kilichofanyika Juni 29, 2018 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

Kikao hicho kimejadili na kutoa mwongozo wa masuala yatakayojadiliwa katika kikao cha Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT) na Wawekezaji wa Mradi husika.

Viongozi wa Serikali, wakiwemo Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali, wameshiriki kikao hicho muhimu.

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, pia ameshiriki kikao hicho.

Viongozi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), wakiwa katika kikao kilichofanyika Juni 29, 2018 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

Na Veronica Simba – Dodoma.