Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara wilayani Chato mkoani Geita ya kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu ( REA III).

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Butarama wilayani Chato mkoani Geita.

Akiwa wilayani humo amezindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bupandwampuli, Kikumbaitale na Butarama.

Vijiji 74 wilayani Chato vipo katika mpango wa kupelekewa umeme kupitia REA III ambapo mpaka kufikia tarehe 27 Oktoba, 2018,   Vijiji 20 vimeunganishwa na huduma hiyo.

Na Teresia Mhagama

27/10/2018

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Bupandwampuli wilayani Chato mkoani Geita.