Leo tarehe 13 Mei, 2018 wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamefanya ziara katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni vilivyopo mkoani Morogoro. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kampuni ya State Grid iliyopewa kazi hiyo katika mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwasha umeme katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni tarehe 16 Mei, 2018.

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ziara hiyo. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Yusuph Msembele.