Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani leo tarehe 12 Novemba, 2018 amevunja rasmi Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Gideona Kaunda.

Uamuzi huo ameutoa katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma.

Alisema kuwa, Bodi hiyo iliundwa mwaka 2017, kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini Na.8 ya Mwaka 2005 (The Rural Energy Act. No.8 of 2005).

“ Bodi hii imetekeleza  majukumu yake kwa takriban mwaka mmoja (1) sasa na katika kipindi hicho ambapo Bodi hii imekuwepo,  ninapenda kuwajulisha kwamba kwa ujumla sijaridhishwa na utendaji wake,” alisema Dkt Kalemani.

Hivyo alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 9(3)(b)  cha Sheria Na. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005,  ameamua kuivunja Bodi hiyo kwa   kutengua uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi.

Aliongeza kuwa, Bodi nyingine mpya  itaundwa baadaye kwa mujibu  wa Sheria  ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.

Bodi hiyo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017 na ina wajumbe Saba.

windows 7 enterprise kaufen