Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI MH...

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI MHE. JANUARY MAKAMBA WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO NA MAENDELEO YA SEKTA YA NISHATI KATIKAMIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATIMHE. JANUARY MAKAMBA WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO NA MAENDELEO YA SEKTA YA NISHATI KATIKAMIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Ndugu Wanahabari,

Sekta ya Nishati ina historia ndefu kuanzia kipindi cha kabla ya kupata Uhuru wetu mwaka 1961 hadi kufikia kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Taifa letu. Sekta hii imepitia maadiliko mbalimbali ya kimuundo, kisheria na kisera yakiwa na lengo la kuiboresha Sekta hii ili iweze kutoa huduma bora kwa watanzania. Wizara inayosimamia Sekta ya Nishati kwa mara ya kwanza iliundwa mwaka 1961 na iliitwa Wizara ya Biashara, Madini na Nguvu za Umeme, hata hivyo sekta ya nishati imekuwa ikitenganishwa au kuunganishwa na kuunda Wizara mbalimbali kutokana na mahitaji ya wakati husika.

Majina ya Wizara zilizohusisha sekta ya nishatikwa nyakati mbalimbali ni Wizara ya Biashara, Madini na Nguvu za Umeme (1961 – 1963); Wizara ya Viwanda, Madini na Nguvu Za Umeme (1963 -1965); Wizara ya Maji na Nguvu za Umeme (1970 – 1975);Wizara ya Maji, Nishati na Madini (1975 – 1980); Wizara ya Maji na Nishati (1980 - 1984); Wizara ya Maji, Nishati na Madini (1984 - 1985); Wizara ya Nishati na Madini (1985 - 1990); Wizara ya Maji, Nishati na Madini (1990 - 1995); Wizara ya Nishati na Madini (1995 – 2017); na Wizara ya Nishati (2017 mpaka Sasa).

Ndugu Wanahabari,

Mawaziri waliowahi kuongoza Wizara zinazohusu Sekta ya Nishati ni: Bw. A. H. Jamal, Bw. J. S. Kasambala, Bw. A. Z. Nsilo Swai, I. Elinawinga, Dkt. W. K. Chagula, Bw. Alnoor Kassum, Bw. John Samwel Malecela, Bw. Jackson Makweta, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Dkt. William Shija, Bw. Edgar Diones Maokola Majogo, Dkt. Abdallah Omari Kigoda, Bw. Daniel Yona, Bw. Ibrahim Msabaha, Bw. Nazir Mustapha Karamagi, Bw. Wiliam Mganga Ngeleja, Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Bw. George Simbachawene, Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Dkt. Medard Matogoro Kalemani na Waziri wa sasa ni Mhe. Bw. January Makamba.

Mawaziri Wadogo ambao wamewahi kutumika kumaanisha cheo cha sasa cha Naibu Waziri. Manaibu Waziri waliowahi kuongoza Wizara zinazohusu Sekta za Nishati na Madini ni: Bw. J. A. Mhaville, Bw. K. H. Ameir, Bw. Al-Noor Kassum, Bw. Mustapha C. Nyang’anyi, Bw. Manju Msambya, Bw. Edgar Diones Maokola Majogo, Meja Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Ernest K. Nyanda, Mhe. Joseph F. Mbwiliza, Bw. Benard Membe, Bw. Lawrence Masha na Bw. Wiliam Mganga Ngeleja, Bw. Adam K. A. Malima, Bw. George Simbachawene, Bw. Steven Masele, Bw. Charles Kitwanga, Bw. Charles Mwijage, Dkt Medard Kalemani, Bi. Subira Mgalu na Naibu Waziri wa sasa ni Mhe. Wakili Stephen Byabato.

Makatibu Wakuu waliowahi kuongoza Wizara zinazohusu Sekta za Nishati na Madini ni: Bw. H. Halwenge, Bw. Jacob Dickson Namfua, Bw. Amon James Nsekela, Bw. Frederick Kilibata Lwegarulila, Bw. Harith Bakari Mwapachu, Bw. Athumani Iddi Janguo, Bw. Samweli Rwakatare, Bw. Fulgence Michael Kazaura, Bw. Paul. J. Mkanga, Prof. Mark Mwandosya, Dkt. Ben Moshi, Bw. Rafael O. S. Mollel, Dkt. Jonas P. Kipokola, Bw. Patrick Rutabanzibwa, Bw. Arthur G. K. Mwakapugi, Bw. David Kitundu Jairo, Bw. Eliakim Maswi, Prof. Justin Ntalikwa, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Mha. Zena Said na Katibu Mkuu wa sasa ni Mha. Leonard R. Masanja.

Ndugu Wanahabari,

Wizara ya Nishati ina Dira na Dhima kama ifuatavyo:

Dira

na inayojali tija ili kuhakikisha kuwa rasilimali za nishati zinachangia ipasavyo katika maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi.

Dhima

Kuendeleza, kudhibiti na kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za nishati kwa manufaa ya Watanzania.

Malengo

Wizara ya Nishati imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Wizara wenye malengo makuu sita (6) kama ifuatavyo:

Ndugu Wanahabari,

SEKTA YA UMEME NA NISHATI JADIDIFU

Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Umeme na Nishati Jadidifu ni pamoja na:

Kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme nchini. Hadi kufikia Mwezi Septemba, 2021 upatikanaji wa umeme umefikia MW 1,609.91 ikilinganishwa na MW 17.5 kabla ya Uhuru. Mahitaji ya juu ya umeme nchini (peak demand) yamefikia MW 1,273.42 mwezi Oktoba, 2021. Uwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyoungwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa umefikia MW 1,573.65 ambapo umeme wa nguvu ya maji (36.46%); gesi asilia 57.28(%); Mafuta (5.60%); na Tungamotaka (Biomass) (0.67%). Uwezo wa mitambo hiyo unajumuisha mitambo inayomilikiwa na TANESCO ambayo huchangia (86.57%) na mitambo ya wazalishaji binafsi (IPPs/SPPs) ambayo huchangia (13.43%).

Uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo nje ya Gridi ya Taifa (off-grid) ni MW 36.26 ambapo TANESCO inamiliki mitambo yenye MW 32.21 na mzalishaji binafsi NextGen Solawazi (Kigoma) MW 5 kwa kutumia nguvu ya jua.

Kukamilika kwa mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji ya: Hale MW 21 (mwaka 1964) na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 11 kutoka Hale hadi Dar es salaam; Nyumba ya Mungu MW 8 (mwaka 1968) na njia ya umeme ya msongo wa kV 66 Kutoka nyumba ya Mungu hadi Arusha; Kidatu MW 204 (mwaka 1975- 1981); Mtera MW 80 (mwaka 1988); New Pangani Falls MW 68 (mwaka 1995); na kihansi wa MW 180 (mwaka 2000).

Kukamilika kwa ujenzi wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asili ya: Songas MW 189 (mwaka 2004); Ubungo I MW 102 (mwaka 2008); Ubungo II MW 105 (mwaka 2012); Tegeta MW 45 (mwaka 2009); Somanga Fungu MW 7.5 (mwaka 2010); Kinyerezi I MW 150 (mwaka 2016) na ujenzi wa njia za umeme wa kV 220 (Kinyerezi - Kimara) na kV 132 (Kinyerezi - Gongolamboto); Nyakato MW 63 (mwaka 2013), Kinyerezi II MW 248 (mwaka 2018) na Mtwara gas power plant MW 22 (mwaka 2019).

Kukamilika kwa ujenzi wa njia za kusafirisha umeme za: kV 66 yenye urefu wa Kilomita 125 kutoka Mbala, Zambia hadi Sumbawanga (mwaka 2001); kV 220 kutoka Singida na Arusha (mwaka 1996) km 300; kV 132 kutoka Ubungo-Makumbusho (mwaka 2010) kilomita 7; kV 132 yenye urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mahumbika (Lindi) pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Mtwara na Mahumbika; kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Singida km 670 (mwaka 2016), kV 220 kutoka Makambako hadi Songea km 250 pamoja na ujenzi wa vituo vitatu (3) vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea (mwaka 2018); na kV 220 Bulyanhuku Geita km 55 (mwaka 2020).

vijiji 8,897 kupatiwa umeme kati ya vijiji vyote 12,345 na kubakia na vijiji 3,448 visivyokuwa na huduma ya umeme; Kuendelea kuunganisha umeme wateja wapya nchini kwa kasi ambapo hadi Juni, 2021 jumla ya Watanzania wanaotumia nishati ya umeme wameongezeka kufikia takriban milioni 47 sawa na asilimia 78 ya Watanzania wapatao milioni 60.

kupoza umeme kwa ajili ya kuboresha upatikanaji na umeme vya Mbagala, Kipawa, Gongolamboto na Mburahati Mkoani Dar es Salaam; vituo vya kupoza umeme vya Njiro B, Mount Meru, Sakina, Unga Ltd, Kiltex na Themi Mkoani Arusha; vituo vya kupoza umeme vya Bomambuzi na Trade School Mkoani Kilimanjaro; ukarabati wa vituo vya kupoza umeme vya Mikocheni, Oysterbay, City Centre, Gongolamboto, Kariakoo, Mbagala, Chang’ombe, Kipawa na Ubungo Mkoani Dar es Salaam.

Kukamilika kwa ujenzi wa vituo vipya vya kupoza umeme vya Mbagala, Kipawa, Gongolamboto na Mburahati Mkoani Dar es Salaam; Njiro B, Mount Meru, Sakina, Unga Ltd, Kiltex na Themi Mkoani Arusha; Bomambuzi na Trade School Mkoani Kilimanjaro; Kukamilika kwa ukarabati wa vituo vya kupoza umeme vya Mikocheni, Oysterbay, City Centre, Gongolamboto, Kariakoo, Mbagala, Chang’ombe, Kipawa na Ubungo Mkoani Dar es Salaam; kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha Dege, Kigamboni 132/33 kV pamoja na njia ya kV 132 toka Kibada hadi Dege.

kwa ajili ya kusambaza umeme katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe na Tanga kwa ufadhili wa Millenium Challenge Corporation (MCC).

.

Kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme wa Electricity V (2015) katika Wilaya za Bukombe, Kwimba, Magu, Mbogwe, Misungwi na Sengerema. Mradi huo ulihusu ujenzi wa njia ya kusambaza umeme wa Msongo wa kV 33, kufunga transfoma na kuwaunganishia umeme wateja 8,600.

Kujengwa na kukamilika “submarine cable” mbili zilizopita chini ya bahari zenye msongo vya Kilovoti 132 na kV 33 kwenda Visiwa vya Unguja na Pemba kV33 sawia.

Kukamilika kwa Sera, Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya Nishati: Sera ya Taifa ya Nishati 1992, 2003 na 2015, Sheria ya Umeme ya Mwaka 2008 na mabadiliko yake ya Mwaka 2020, Sheria ya Wakala wa Nishati Vijijini (2005), Sheria ya Mamlaka ya kuthibiti na Huduma za Nishati na Maji, (2001); Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme (Power System Master Plan) wa Mwaka 2008, 2012, 2016 na 2020, Mkakati na Mwelekeo wa Maboresho katika Sekta Ndogo ya Umeme (Electricity Supply Industry Reform Strategy and Action Plan (2014 – 2025), Programu ya Nishati Endelevu kwa Wote (Sustainable Energy for ALL (SE4ALL) Action Agenda 2015, Programu ya Umeme Vijijini (Rural Electrification Programu) 2016 na Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia (Natural Gas Utilization Master Plan – NGUMP) 2016.

Kukamilisha kwa Kanuni (Rules) mbalimbali kwa ajili ya Udhibiti huduma za nishati. Kanuni hizo ni pamoja na:Kanuni za Uendelezaji na Usimamizi wa Miradi Midogo ya Umeme (The Electricity (Development of Small Power Projects) Rules, 2016, GN No. 217 of 2016); Kanuni za Tozo na Ada za Leseni za Umeme (The Electricity (Licensing Fees) Rules, 2016, GN No.287 of 2016); Kanuni za Usimamizi wa Mifumo ya Umeme (The Electricity (System Operation Services) Rules, 2016, GN No. 324 of 2016); Kanuni za Usimamizi wa Soko la Biashara ya Umeme (The Electricity (Market Operation Services) Rules, 2016, GN No. 325 of2016); Kanuni za kusimamia Uuzaji umeme (The Electricity (Supply Services) Rules, 2017, GN No. 4 of 2017); na Usimamizi wa Biashara ya Rejareja ya Petroli Vijijini na kwenye Miji Midogo (The Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) Rules, 2017, GN No. 14 of 2017).

Kuongezeka kwa kiwango cha upatikanaji umeme nchini.overall electricity access level) Tanzania Bara kimeongezeka na kufikia asilimia 78.4, ambapo mijini (urban electricity access level) imefikia asilimia 99.6 na vijijini (rural electricity access level) takriban asilimia 69.8.

Kuongezeka kwa idadi ya Taasisi zilizopatiwa umeme vijijini. Hadi kufikia mwezi Machi, 2020 jumla ya Taasisi na maeneo ya umma 15,200 yamepatiwa umeme chini ya Mpango wa REA ambapo taasisi za elimu (4,036), maeneo ya biashara (5,053), visima/mashine za maji (338), taasisi za afya (1,296) na nyumba za ibada (1,113).

Kuandaliwa na kuanza kutumika kwa mikataba mahsusi ya kuuziana umeme (Standardized Power Purchase Agreement - SPPA) kwa wawekezaji wadogo inayotoa mwongozo wa bei (Standandadized Power Purchase Tariff - SPPT), ambapo wawekezaji watano (5) - (TANWAT-MW 2.75, TPC-MW 20, Sao Hill-MW 16, Ngombeni-MW 0.5 na Mwenga-MW 3.36), wamepewa leseni za kuzalisha umeme wenye jumla ya MW 42.61.

Kukamilika kwa Mradi wa kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme katika Jiji la Dar es Salaam. Mradi ulihusisha: ukarabati wa Kituo cha Ilala kV 132/33/11; ujenzi wa Jengo Jipya la “Control Center” la Ilala; ufungaji wa njia ya pili ya usafirishaji umeme wa Msongo wa kV 132 kutoka Ubungo hadi Ilala; kupanua Kituo cha kupoza umeme cha Msasani kV 33/11; ujenzi wa Vituo Vipya vinne (4) vya kupoza umeme wa kV 33/11 vya Jangwani Beach, Mwananyamala, Msasani na Muhimbili; ujenzi wa njia mpya za Msongo wa kV 33 kutoka Vituo vya kupoza umeme vya Makumbusho, City Centre na Tegeta kwenda Vituo Vipya vya Mwananyamala, Muhimbili, Jangwani na Msasani;.

utekelezaji wa Programu ya Awamu ya Pili ya Mradi wa Sustainable Solar Market Package (SSMP – II) (2016). Mradi ilihusu ujenzi wa Mifumo ya Umeme Jua katika Wilaya nane (8) za Biharamulo, Bukombe, Chato, Kasulu, Kibondo, Namtumbo, Sikonge na Tunduru na kufungwa Jumla ya Mifumo Midogo ya Umeme 4,620 yenye uwezo wa kWp 115.

Kuunganishwa kwa Mikoa katika Gridi ya Taifa. Hadi kufikia Mwezi Septemmba, 2021 mikoa yote ya Tanzania Bara ilikuwa imeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa isipokuwa mikoa minne tu ya Kigoma, Katavi, Rukwa; baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera. Hata hivyo, Mkoa na Kagera wanapata umeme kutoka nchi za Zambia na Uganda sawia.

Kusitisha matumizi ya mitambo ya kukodi ya binafsi ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito katika kuzalisha umeme ikiwemo ya Aggreko na IPTL na kuokoa wastani wa jumla ya Shilingi bilioni 11.46 kwa mwezi.

Kusitisha uingizaji wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo, transfoma, nyaya na mita za LUKU ndani ya nchi na Kuendelea na kuhamasisha uzalishaji wa vifaa vya kuunganisha umeme hapa nchini na kuokoa wastani wa Shilingi bilioni 162.57 kwa mwaka.

Kugunduliwa kwa maeneo yanayoweza kuzalisha umeme kutokana na jotoardhi katika maeneo ya Songwe (Mbeya), Ziwa Manyara (Manyara), Maziwa Eyasi na Natron (Arusha), Luhoi (Rufiji-Pwani), ambapo takriban kati ya MW 150 – 650 zinaweza kuzalishwa, hivyo kuongeza vyanzo vya nishati nchini.

Kuwezesha matumizi ya umeme wa jua katika maeneo ya huduma za kijamii kama zahanati, shule za sekondari na taa za barabarani katika wilaya ya Sumbawanga vijijini kupitia mradi mkubwa wa umeme wa jua (Sustainable Solar Market Packages).

Ndugu Wanahabari, Mafaniko mengine kwa upande wa Sekta ya Umeme na Nishati Jadidifu ni:

asilimia 45.58; Kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Rusumo MW 80 ambao hadi Mwezi Septemba umefikia asilimia 82 na kuanza maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya kufua umeme ya Ruhudji (MW 358) na Rumakali (MW 222);

asilimia 82 na kuanza maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya kufua umeme ya Ruhudji (MW 358) na Rumakali (MW 222);

SEKTA YA MAFUTA NA GESI

Ndugu Wanahabari,

Kabla ya uhuru biashara ya mafuta ilianza maeneo ya mwambao wakati Bw. Smith MacKenzie alipoanza kuingiza mafuta kwenye visiwa vya Zanzibar kama wakala wa Kampuni ya Shell. Kampuni hiyo ilipanua shughuli zake hadi maeneo ya Tanzania Bara na pia ilijihusisha na utafutaji wa mafuta hadi mwaka 1964.

Mwaka 1966, Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Agip iliunda kampuni ya Tanzania and Italian Petroleum Refinery (TIPER) ambayo ilihusika na kuagiza, kusafisha na kuuza mafuta kwa kampuni za usambazaji. Hata hivyo, kiasi cha mafuta kilichokuwa kinasafishwa na kampuni hiyo hakikukidhi mahitaji. Kutokana na sababu hiyo, mwaka 1969 Serikali ilianzisha Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969 iliyotolewa kwenye Government Notice Na. 140 ya tarehe 30 Mei, 1969 na kuanza rasmi shughuli zake mwaka wa fedha 1973/74. TPDC pia ilikuwa na jukumu la kusimamia shughuli za utafiti wa awali na utafutaji mafuta kwa kushirikiana na kampuni nyingine chini ya mikataba ya Production Sharing Agreement (PSA).

Ndugu Wanahabari,

Serikali ilitoa leseni ya utafutaji wa mafuta ya petroli kwa Kampuni ya AGIP katika eneo la mwambao wa bahari ya Hindi kutoka Mtwara hadi Tanga. Shughuli za utafutaji wa mafuta zilianza rasmi mwaka 1973 na kampuni hiyo ikagundua gesi asilia katika eneo la Songo Songo mwaka 1974. Kwa kuwa lengo lilikuwa ni kupata mafuta, AGIP ilirudisha eneo hilo kwa Serikali mwaka 1975 na kuendelea na utafutaji wa mafuta. Wakati AGIP ikiendelea na juhudi za utafutaji mafuta, TPDC ilianza rasmi shughuli za uagizaji mafuta ghafi mwaka 1977. Mwaka 1980, Sheria ya Utafutaji na Uendelezaji wa Mafuta (Petroleum Exploration and Production Act, 1980) ilitungwa ili kuwezesha mikakati ya Serikali ya kuhamasisha ushiriki wa kampuni za kimataifa. Mwanzoni mwa miaka ya 1980, Serikali iliingia mikataba ya utafutaji (PSA) na kampuni za Shell, ELF, AMOCO na International Energy Development of America. Mwaka 1982, Kampuni ya AGIP iligundua tena gesi asilia katika eneo la Mnazi Bay na kurudisha eneo hilo kwa Serikali. Kwa upande wa mafuta, Serikali kupitia TPDC ilikuwa na utaratibu wa kuagiza mafuta ghafi na kuyasafisha nchini katika kiwanda cha TIPER. Kwa kuwa kiasi cha mafuta kilichosafishwa nchini hakikukidhi mahitaji, TPDC ilianza kuagiza mafuta yaliyosafishwa Mwaka 1983.

Utafiti uliofanyika mwaka 1990 ulionesha kuwa eneo la Songo Songo lina hifadhi ya gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 540. Aidha, gesi hiyo ilionekana kuwa na ubora wa hali ya juu kwa kuwa na kiasi kikubwa cha gesi ya methane, kutokuwa na sulphur na kuwa na kiasi kidogo cha maji. Serikali kupitia TPDC iliingia mkataba na kampuni ya mafuta ya India (ONGC) ya kuchimba visima vitatu katika eneo hilo ili kuhakiki kiasi cha gesi asilia kilichopo.

Songo-Songo Gas to Electricity Project). Lengo la Serikali lilikuwa kutekeleza mradi huu kwa kutumia wawekezaji binafsi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea katika ujenzi na uendeshaji. Mwaka 1994, kupitia utaratibu wa ushindani, Serikali iliichagua Kampuni ya Ocelot Energy Inc. na TransCanada Pipelines Ltd (OTC) consortium kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa Songo-Songo. Mkataba kati ya Serikali na Kampuni hiyo wa kuendeleza mradi ulisainiwa mwezi Oktoba, 1995. Kwa upande mwingine, Serikali ilifanya majadiliano na kampuni za World Wide Exploration (Australia), Dublin International Petroleum Ltd (Ireland), Kisoa (Dubai) na Hunt United (USA) kwa ajili ya utafutaji mafuta na gesi kwenye maeneo yaliyotarajiwa kupitishwa bomba la gesi. Kampuni hizo hazikuweza kugundua chochote.

Ndugu Wanahabari,

Mwaka 1996-2000 Serikali ilianzisha taratibu za kuwa na soko huria katika biashara ya mafuta ili kuleta ushindani ambao utarahisisha upatikanaji na unafuu wa bei za mafuta na bidhaa zake. Pamoja na kuanzishwa kwa soko huria bei za mafuta ziliendelea kupanda kiholela na kuleta adha kwa watumiaji. Kufuatia hali hiyo, mwaka 2006 Serikali iliunda Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Energy and Water Utilities Regulatory Authority-EWURA).

Kuanzishwa kwa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, kuanzishwa kwa Taasisi ya Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), kuwepo kwa Kanuni za utekelezaji kama vile za Bei ya Gesi Asilia, Ushirikishwaji wa Wazawa (Local Content Regulations), Ukusanyaji wa Tozo zitokanazo na mauzo ya gesi asilia (Annual levy – Fee and Charges), kumeimarisha utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli za utafutaji mafuta na uzalishaji gesi asilia hapa nchini. Usimamizi wa sekta umezidi kuimarika baada ya kuwepo Sheria na Kanuni hizi ambazo zimeandaliwa na kupitishwa ndani ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.

Serikali iliweka mikakati ya kuhamasisha ushiriki wa wazawa katika shughuli za mafuta na gesi na hadi kufikia mwaka 2015 idadi ya wazawa iliongezeka maradufu katika kazi za utafutaji mafuta na gesi na uzalishaji wa gesi asilia. Kwa mfano, idadi ya wazawa walioshiriki katika uchimbaji wa kisima cha Kitatange-1 katika bahari kuu mwaka 2016 walikuwa nane (8), wakati wazawa wapatao 58 kati ya wafanyakazi 160 waliokuwepo, walishiriki katika uchimbaji wa kisima cha Pilipili-1 kilichochimbwa katika bahari kuu mwaka 2018. Idadi ya wazawa walioajiriwa na kuchukuwa nafasi mbalimbali za uongozi katika Makampuni ya kigeni yanayotekeleza shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi asilia hapa nchini imeongezeka. Kwa mfano, Katika kampuni la Statoil na Shell, idadi ya wazawa walioajiriwa katika nafasi za uongozi walikuwa chini ya asilimia 50%, wakati kwa mwaka 2020 imefika zaidi ya asilimia 90%.

Ndugu Wanahabari,

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015, Kampuni ya Mafuta ya Taifa (TPDC) imeanza kushiriki moja kwa moja katika utafutaji wa mafuta katika eneo la Eyasi Wembere lililopo katika Mikoa ya Tabora, Manyara na Simiyu kwa kutumia wataalamu wa ndani. Katika eneo la Eyasi Wembele, TPDC imefanikiwa kuchoronga visima viwili (2) vifupi (shallow borehole) vya utafiti wa awali, na inatarajia kuchoronga kisima kimoja (1) mwanzoni mwa Mwezi July 2020, hivyo kupelekea kuwa na jumla ya visima vitatu (3) katika eneo hilo. Pia, kwa sasa TPDC ipo katika maandalizi ya kuchoronga visima vya utafutaji wa mafuta na gesi katika Kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini.

Mafanikio katika Sekta ya Mafuta na Gesi

Ndugu Wanahabari,

Tangu kupatikana kwa uhuru, Serikali imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuiwezesha Sekta Mafuta na Gesi iweze kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya nchi. Katika kipindi hicho mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwa ni pamoja na:

(a)Trilioni 57.54 mwaka 2021. Ugunduzi huo umewezesha kuanza kutumika kwa gesi asilia kama chanzo cha nishati, hususan kwa kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na kwenye magari.

(b)52 Jijini Dar es Salaam, Mkoani Pwani na Mtwara vinatumia gesi asilia. Aidha, vituo viwili vya kushindilia na kujazia gesi asilia kwenye magari jijini Dar es Salaam na Mtwara vinafanya kazi.

(c)asilimia 60 ya umeme unazalishwa kwa kutumia gesi asilia.

(d)Shilingi Trilioni 38 ambazo zingetumika kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya mitambo ya umeme na ya viwandani.

(e)Shilingi bilioni 208 katika Mfuko wa Mafuta na Gesi kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 baada ya kukamilika Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mtwara/ Songosongo hadi Dar es Salaam.

(f)shilingi bilioni 441 yanayotokana na kodi mbalimbali kuanzia mwaka 2015 baada ya kukamilika kwa mradi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mtwara/ Songosongo hadi Dar es salaam.

(g)shilingi bilioni 10 katika mwaka 2018/2019 na mwaka 2019/20 ikiwa ni gawio (Dividend) kwa Serikali.

(h)Magari 750 yamewekewa mfumo wa matumizi ya nishati ya gesi asilia.

(i)

shilingi bilioni 462 huokolewa kila mwaka ikilinganishwa na kabla ya mfumo husikakuanza kutumika;

takribani bilioni 391 huokolewa kila mwaka ikilinganishwa demurrage zilizokuwa zikilipwa kabla ya mfumo wa BPS.

(j)shilingi bilioni 35.91.

(k) (indicative price) na bei kikomo (cap price) katika biashara ya mafuta ya jumla na rejareja unafanyika kupitia mamlaka hiyo. Hatua hii imezingatia maslahi ya mtumiaji na muuzaji.

(l) 1,000 zimeorodheshwa katika kanzidata inayomilikiwa na EWURA ikishirikiana na PURA iliyowezesha kampuni hizo kushiriki katika miradi mbalimbali.

(m)

(n)

(o)

(p)

(q)asilimia 19.2 mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa asilimia 4 mwezi Machi, 2020.

(r)Shilingi trilioni 8.1. Hadi sasa Serikali imewezesha Kusainiwa kwa Mkataba kati ya Nchi Hodhi na Wawekezaji (Host Government Agreement – HGA); Kusainiwa kwa Mkataba wa Ubia baina ya Wawekezaji (Shareholders’ Agreement – SHA); Kukamilika kwa majadiliano na kuridhiwa kusainiwa kwa Mikataba ya uendeshaji wa Bandari ya Chongoleani na Mikataba ya ukodishaji wa ardhi ya mradi kwa maeneo ya kipaumbele na mkuza wa bomba; Kukamilika kwa malipo ya fidia kwa eneo la Chongoleani itakapojengwa Bandari;Kuendelea na ulipaji wa fidia kwa Wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi; Utoaji wa elimu kwa wananchi katika maeneo yanayopitiwa na mradi ni kazi endelevu; na Kusainiwa kwa mkataba wa nchi zinazotekeleza mradi (Intergovernmental Agreement-IGA).

(s)

(t)

(u)

(v)

HITIMISHO