The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

ASILIMIA 10 YA GESI ASILIA ILI...

ASILIMIA 10 YA GESI ASILIA ILIYOGUNDULIWA AFRIKA INAPATIKANA TANZANIA.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, anayeshughulikia masuala ya Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio ameeleza kuwa asilimia 10 gesi asilia iliyogundulika na ambayo haijaendelezwa Afrika inapatikana Tanzania.

Dkt. Mataragio amesema hayo alipotembelea mabanda ya maonesho katika Wiki ya Nishati inayoendelea katika viwanja vya Bunge, Jijini Dodoma Aprili 21, 2026.

Dkt.Mataragio amefafanua kuwa gesi iliyogundulika na ambayo haijaendelezwa Afrika inafikia futi za ujazo trilioni 550, ambapo Tanzania ina futi za ujazo trilioni 57 ambayo ni asilimia kumi ya gesi hiyo iliyogundulika Afrika.

Amesema kutokana na wingi wa gesi inayopatikana nchini, Tanzania sasa inajukumu la kuongeza kasi ya matumizi ikiwemo uzalishaji wa umeme, kuongeza kasi ya matumizi ya gesi katika kuendesha viwanda, vyombo vya moto na kutumika katika nishati safi ya kupikia ambapo ifikapo mwaka 2034, asilimia 80% ya Watanzania watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia.