BADO HUJACHELEWA!
Tabasamu, huduma bora na elimu sahihi vinakusubiri katika Banda la Wizara ya Nishati kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Fika uzungumze moja kwa moja na wataalamu wetu, upate majibu ya maswali yako, ujifunze kuhusu nishati safi ya kupikia, umeme, mafuta, gesi asilia, pamoja na huduma, miradi na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.
Tunakukaribisha leo kutembelea Banda la Wizara ya Nishati lililopo karibu na jengo la TANESCO, Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Karibu ujionee, ujifunze na upate huduma zote sehemu moja!