BANDA LA WIZARA YA NISHATI LAENDELEA KUVUTIA WADAU KATIKA WIKI YA MAZINGIRA.
Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Wiki ya Mazingira yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), jijini Dodoma, ambapo wamepata fursa ya kujionea mafanikio na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.
Katika banda hilo, wageni mbalimbali wamejionea gari linalotumia umeme kwa asilimia 100 aina ya Nissan Leaf pamoja na kupata elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, maendeleo ya umeme vijijini na mijini, na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara ya Nishati na taasisi zake.
Karibu utembelee banda la Wizara ya Nishati kupata elimu na taarifa muhimu kuhusu sekta ya nishati.
Aidha maonesho ya Wiki ya Mazingingira yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 5 Juni 2026.