Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

BUNGE LARIDHIA KUJIUNGA NA MKA...

BUNGE LARIDHIA KUJIUNGA NA MKATABA WA NISHATI JADIDIFU

Leo Oktoba 31, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia Tanzania kujiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu (IRENA).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Tanzania itanufaika na mkataba huo na itachangia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na uharibifu wa mazingira.

Dk. Biteko ameongeza kuwa malengo ya mkataba huo ni kuhamasisha matumizi endelevu ya nishati jadidifu.

Aidha Dk. Biteko amesema kuimarika kwa nishati jadidifu katika uzalishaji wa nishati ya umeme utaliwezesha taifa kuwa na vyanzo vya mchanganyiko wa umeme unaoendana na mahitaji ya ukuaji wa uchumi na jamii.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini Dk. David Mathayo ameishauri wizara ya nishati kuhakikisha wataalamu wa kuzalisha nishati hiyo wanapatikana

Wakala wa kimataifa wa nishati jadidifu Ulianzishwa mwaka 2009 ambapo Tanzania ilisaini mkataba huu lakini haikuridhia azimio la mkataba huo kwa lengo la kujiridhisha namna ya utekelezaji wake.