Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

Byabato ashiriki kikao cha Maw...

Byabato ashiriki kikao cha Mawaziri wa Nishati Afrika.

Na Timotheo Mathayo, Dodoma.

Naibu wa Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameshiriki kikao cha Mawaziri wa Sekta ya Miundombinu na Nishati wa nchini za Afrika.

Kikao hicho kimefanyika Juni 16, 2022 kwa njia ya mtandao na kimezungumzia maendeleo ya Sekta ya Nishati katika Bara la Afrika.

Amesema kuwa vita ya Ukraine na Urusi imeleta madhara na kusababisha bei ya bidhaa kama Mafuta kupanda pamoja na gharama usafirishaji.

Wakili Byabato amesema lengo la kikao hicho maalum ilikuwa ni kujadili athari za vita vya Ukraine na Urusi katika Sekta ya Nishati kwa nchi za Afrika, jambo ambalo limewafanya Mawaziri kujadili namna bora ya kukabiliana na athari zilizojitokeza kutokana na vita hivyo.

Hata hivyo imejulishwa kuwa hivi sasa Dunia inahama kutoka kwenye matumizi ya Nishati chafu kwenda Matumizi ya Nishati safi kama Gesi na Umeme.

"Moja ya makubaliano tuliyofikia katika kikao hicho ni kuongeza kasi ya kujenga Miundombinu ya Gesi katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ili tunufaike na masuala ya Nishati mbadala" amesema Byabato.

Pia Wakili Byabato, amesema kuwa katika kutatua changamoto za sasa Afrika inabidi kuona namna nzuri yakuagiza mafuta kwa kushirikiana ili kupunguza makali ya Bei za mafuta.

Aidha katika kikao hicho imebainishwa kuwa katika mataifa ya Ulaya Gesi inahitajika sana katika shughuli mbalimbali kama kupikia, viwandani na kwenye shughuli za usafirishaji pamoja na maeneo mengine kutokana na vita inayoendelea.

Mawaziri wa Nishati wa nchi za Afrika wamekubaliana kuwa Afrika inaweza kuwa chanzo cha Nishati, hususan Gesi kwa ajili ya kuuza nchi za Ulaya na wamepitisha mpango ujulikanao kama Afrika Energy Security Plan (AESP).

Kuhusu Sekta ya Usafirishaji wamekubaliana kuimarisha na kutumia Miundombinu ya Treni za Umeme pamoja na Magari ya kutumia Nishati ya Umeme ili kuepuka gharama ya bei ya Mafuta pamoja na uchafuzi wa mazingira.