Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

DKT. BITEKO MGENI RASMI NISHAT...

DKT. BITEKO MGENI RASMI NISHATI BONANZA 2025

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Wizara ya Nishati na Taasisi zake litakalofanyika jumamosi Juni28, 2025jijini Dodoma.

Akizungumzia maandalizi ya Bonanza hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Bi. Neema Mbuja amesema kuwa, Nishati Bonanza litafanyika kwenye Viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma na kushirikisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na wadau kutoka Wizara nyingine.

‘’ Nipende kuchukua fursa hii kuzikaribisha taasisi zilizo chini yaWizara ya Nishatikushiriki kikamilifubonanza ambalo linaleta fursa ya kufahamiana na kubadilishana mawazo baada ya muda wa kazi pamoja nakufanya mazoezi ili kujenga afya." Amesema Mbuja

Ameongeza kuwa, kwamwaka huu Nishati Bonanzalinaongozwa na kauli mbiu ya "Michezo kwa Afya bora, Shiriki uchaguzi 2025 ikiwa na lengo pia la kuhamasisha wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 .

Amesema maandalizi yote yameshakamilika na timu zitakazoshiriki michezo mbalimbali zimeshawasili Dodoma kushiriki bonanza hilo litakaloshirikisha watu takribani 1000.

Ametaja michezo itakayoshindaniwa kuwa nini pamoja na Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Wavu, Mpira wa Kikapu, Kuvuta Kamba, pamoja namichezo ya jadi kama vile bao na drafti, piakufukuza kuku.

Taasisi zitakazoshiriki Bonanza hilo laNishati ni pamoja na TANESCO, REA, TPDC, PURA, EWURA, TGDC, ETDCO, TCPM, TANOIL, GASCO, PBPA.

Hili ni Bonanza la pili kufanyika tangu kuasisiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt Doto Biteko mwaka jana.