The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

KATIBU MKUU MATARAGIO AKUTANA...

KATIBU MKUU MATARAGIO AKUTANA NA UONGOZI ARA PETROLEUM KUJADILI MIRADI YA GESI.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkuu wa ARA Petroleum Tanzania (APT), Erhan Saygi, leo Mei 05, 2026.

Katika kikao hicho, Dkt. Mataragio amepokea taarifa kuhusu maendeleo ya uchimbaji wa gesi katika mradi wa Ntorya pamoja na maandalizi ya kuanza uchimbaji wa visima vipya ambavyo vinatarajia akusaidia kubaini zaidi kiasi cha akiba ya gesi na kuharakisha hatua za uzalishaji.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima, pamoja na wataalamu kutoka Wizara hiyo.