Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

KATIBU MKUU NISHATI ASISITIZA...

KATIBU MKUU NISHATI ASISITIZA UFANISI UTOAJI HUDUMA SEKTA YA NISHATI

Azungumza na Watumishi Wizara ya Nishati

Ataka weledi kazinikuchochea ukuaji Sekta ya Nishati

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha.Felchesmi Mramba ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi katika Wizara hiyo amekutana na kuzungumza na Watumishi kwa ajili ya kusikiliza hoja mbalimbali pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi lengo likiwa ni kuhakikisha Wizara ya Nishati inazidisha ufanisi katika kuwahudumia Watanzania.

Kikao hicho kimefanyika Oktoba 2, 2024 jijini Dodoma na kuwakutanisha Viongozi Wakuu wa Wizara, Menejimenti na Watumishi.

" Tunapotekeleza majukumu yetukila Mtumishi katikasehemu yake ya kazi anatakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi kwa lengo lakuendeleza ukuaji waSekta ya Nishati." Amesema Mha. Mramba

Katika kikao hicho Mhandisi Mramba amewakumbusha Watumishi wa Wizara kuwa Sekta ya Nishati ni nguzo muhimu katika uchumi wa nchi hivyo utendaji kazi mahiri utawezesha sekta kuchangia ukuaji wa uchumi huo.

Amezungumzia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Wizara na kusisitiza kuwa jengo hilo litakuwa na Ofisi za Madereva, hivyo amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutembelea jengo hilo ili kuona hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi.

Mha. Mramba amewataka watumishi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya viungo ili kuendelea kuimarisha afya zao kwa ajili ya kuepuka magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Dkt. Khatibu Kazungu ambaye aliahidiushirikianoili kuhakikisha shughuli mbalimbali katika Wizara ya Nishatizinafanyika kwa lengo la kuchochea maendeleo ya Taifa.