KATIKA SIKUKUU YA SABASABA; NISHATI TUPO TAYARI KUKUHUDUMIA.
Katika kuadhimisha Sikukuu ya Sabasaba, Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake inaendelea kukaribisha wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Wizara ya Nishati na Taasisi zake zinatoa huduma na elimu kuhusu umeme, mafuta, gesi asilia, nishati safi ya kupikia pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika sekta ya nishati.
HERI YA SIKUKUU YA SABASABA; Karibu tukuhudumie.