KENYA, NIGERIA, POLAND, CONGO DRC NA RWANDA KATIKA BANDA LA NISHATI SABASABA.
Ujumbe unaojumuisha nchi mbalimbali ikiwemo Poland, Nigeria, Kenya, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Katika Banda la Wizara ya Nishati, ujumbe huo ulielezwa kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya kikanda inayoendelea kwa upande wa umeme, mafuta na gesi asilia.