Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

KOROGWE WAIPONGEZA SERIKALI UT...

KOROGWE WAIPONGEZA SERIKALI UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME

Ni katika ziara ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga

Vijiji vyote 118 vyafikishiwa umeme

Naibu Waziri Kapinga ashiriki ziara

Wananchi wa Wilaya ya Korogwe wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wa miradiya umeme Vijijini ambapo katika wilaya hiyovijiji vyote vimefikishiwa umeme.

Pongezi hizo zimetolewa kupitia Mbunge wa Korogwe VijijiniMhe. Timotheo Mzava leo Februari 24, 2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Wilayani Korogwe kukagua miradi ya maendeleo.

"Tarehe 15 mwezi wa tatu 2021 ulikuwa kwenye viwanja hivi na sisi wabunge tulipata nafasi ya kusema.Tuliyoyaomba ikiwemo ya umeme vijijini umeyatekeleza tunakushukuru sana." Amesema Mhe. Mzava

Amesema wakati huo wa ziara ya Rais Samia walieleza kuhusu changamoto ya upatikanaji umeme ambapoVijiji 54 kati ya 118 vilikuwa havina umeme.

Mhe. Mzava ameongeza kuwa hivi sasa vijiji vyote 118 vya Korogwe Vijijini vimefikiwa na nishati ya umeme na wananchi wanaendeleakujishughulisha na shughuli za kiuchumi zinazotumia umeme.

Katika ziara hiyo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameshirikiakimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.