Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​Makamba akutana na Viongozi w...

​Makamba akutana na Viongozi waandamiziwa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia

Makamba akutana na Viongozi waandamiziwa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia

Waziri wa Nishati January Makamba amefanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania,Tri Yogo Jotmiko na Viongozi Waandamizi wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Pertamina ya nchini Indonesia akiwemo Rais wa Kampuni hiyo John Anis.

Mazungumzo hayo yamefanyika Mei 16, 2023 jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kuzungumzia suala la kampuni ya Maurel & Prom ambayo inamilikiwa na Kampuni ya Pertamina kwa asilimia 100 kununua hisa za Kampuni ya Wentworth Resources ambaye ni mbia katika Kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara.

Makamba ameileza Kampuni hiyo kuwa Tanzania imeweka mazingira rafiki katika suala zima la uwekezaji hivyo kuhusu maombi yao, ameelekeza Taasisi husika ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (PURA) kutakutana kwa pamoja ili kutazama suala hilo na kuishauri Serikali kama Sheria inavyoelekeza.

Viongozi wengine walioshiriki katika Kikao ni Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Macocha Tembele, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame na Viongozi wengine wandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu (PURA).

Kampuni ya Maurel & Prom imeonesha nia ya kununua hisa za Wentworth Resources ambaye ni mbia mwenza kwenye kitalu cha Mnazi Bay. Ununuzi huo utapelekea mabadiliko katika uendeshaji wa kitalu hicho (change of control) na kuongeza hisa za Maurel & Prom kutoka 48% za sasa hadi 80%, mbia mwingine katika kitalu hiki ni TPDC mwenye asilimia 20 ya hisa.