Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​Makamba awahakikishia soko la...

​Makamba awahakikishia soko la ndani Wadau wa nguzo za umeme

Makamba awahakikishia soko la ndani Wadau wa nguzo za umeme

Ø Aunda Kamati maalum itakayowezesha upatikanaji wa nguzo zenyeubora zaidi

Na Zuena Msuya, Iringa

Waziri wa Nishati, January Makamba amewatoa hofu wadau wanguzo za Miti za umemenchini kwa kuwahakikishia soko la kuuzanguzo zenye uborakwa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA).

Makamba alisema hayo wakati wa mkutano wake uliohusiha Wazalishaji, Wasafirishaji, na Watengenezaji wanguzo za miti za Umeme kutoka Mkoa wa Iringa na Njombe, uliofanyika Mafinga mkoani Iringa, Aprili 30, 2022.

Makamba aliwataka Wadau hao kuzalisha nguzo hizo zenye ubora ili Serikali iweze kuwatafutia masoko ya nje kwa kuwa wana uwezo kuzalisha zaidi kukidhi mahitaji ya soko la ndani ya sasa na ziada.

Mkutano huo ulilenga kuondoa sintofahamu pamoja na minong'ono inayoendelea kwa baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Serikali haitanunua nguzo za Umeme za ndani na badala yake zitaagizwa kutoka nje ya nchi.

Katika mazungumzo yake na Wadau hao, Makamba alisema kuwa, Serikali itaendelea kununua nguzo za miti za Umeme kutoka kwa wazalishaji wake wa ndani ili kulinda viwanda vya ndani kwa kuzingatia ubora wa nguzo uliowekwa.

“Lengo la Serikali ni kukuza uchumi wa wananchi wake kwa kuboresha bidhaa zao kwa kuwasimamia katika kuzalisha kwa vigezo naubora uliowekwa, ili wananchi hao waweze kunufaika na kukuza uchumi wao napato la Taifa kwa ujumla”, Alisema Makamba.

Aliwataka Wadau hao kuhakikisha wanazalisha nguzo zinazokidhi viwango na ubora unaotakiwa kimataifa ili kuweza kukidhi soko la ndani na hata nje ya nchi kwa kuwa mikoa hiyo inaongoza kwa kuwa na uzalishaji wa nguzo.

Alisema kuwa, Serikali itahakikisha kuwa biashara ya nguzo za miti za Umeme, inakuwa zaidi Kitaifa na Kimataifa kama Nchi nyingine zinavyofanya ikiwemo Afrika Kusini ambao wanauza nguzo kama hizo katika nchi nyingine.

Kwa Mantiki hiyo, alielekeza kuundwa kwa Kamatiya watu 12 kutoka katika kila kundi la Wadau wa nguzo za miti za Umeme, katikaMikoa ya Njombe na Iringa,Wizara na Taasisi zake pamoja na Shirika la ViwangoTanzania ( TBS)ili kuongeza ufanisi katika kuzalisha nguzo zenye ubora zinazokidhi viwango.

Kamati hiyo pia itatoa ushauri sahihi kwa Wadau hao juu ya njia bora za kufuata na kuzingatia ili kupata bidhaa zilizobora zitakazo kubalika Kitaifa na Kimataifa.

Waziri Makamba aliwataka Wadau hao kuunda Chama Cha Wazalishaji wa nguzo ili kiweze kudhibiti ubora unaotakiwa na hata kutoa adhabu kali kwa atakayebainika kuzalisha chini ya Kiwango pamoja na kuandaa sheria zitakazoongoza chama hicho.

Aidha aliutaka umoja huo kwenda kujifunza zaidi, namna ya kudhibiti ubora wa nguzo kwa nchi zilizofanikiwa ikiwemo Afrika Kusini ili kuleta ushindani zaidi.

“Ni vyema mkawa na Chama chenu kinachotambulika kisheria, Chama hiki ni chombo muhimu katika kuwasimamia na kuwaongoza, vilevile kitakuwa kinatumika kudhibiti ubora wa nguzo zinazozalishwa kwani atakayekuwa akienda tofauti mtamshughulikia na hata kumpatia adhabu pale atakapokuwa akienda kinyume na kuharibu soko”, alisisitiza Makamba.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Maharage Chande, aliwataka Wadau hao kuwa waaminifu pale nguzo zao zinapotakiwa kupelekwa katika maeneo ya miradi kwa kuweka nguzo halisi zilizokaguliwa na siyo kufanya udanganyifu wa kuweka zisizokuwa na ubora.

Alisema kumekuwa na changamoto ya nguzo kuharibika baada ya muda mfupi kutumika kutokana na kuwa chini ya kiwango na ubora unaotakiwa, huku nguzo hizo zikiwa tayari zimekaguliwa na kuonekana zina ubora unaotakiwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said, aliwahakikishia Wadau hao kuwa soko la nguzo lipo la kutosha kwani bado miradi mingi ya usambazaji wa Umeme vijijini inaendelea na nguzo nyingi zinahitajika.

Akitoa mfano Mkoa wa Iringa kuwa kuna mradi wa ujazilizi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni katika Mkoa huo na mikoa mingine.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, alimuhakikishia Waziri wa Nishati kuwa atashirikiana na Wadau hao kutekeleza yale yanayotakiwa ili kupata bidhaa bora na hatimaye mikoa hiyo iwe kinara katika kuzalisha nguzo na bidhaa za miti zenye ubora unaotakiwa.

Aliwataka Wadau hao kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika na kuwa wasikivu kwa kile watakachokuwa wakielezwa kwa lengo la kupata bidhaa bora kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.