Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

MHE. KAPINGA: TANOIL IMARISHEN...

MHE. KAPINGA: TANOIL IMARISHENI UTENDAJI KAZI KULETA MATOKEO CHANYA

Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni Tanzu ya Mafuta (TANOIL) ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Menejimenti ya Kampuni hiyo wameaswa kuhakikisha kuwa wanaimarisha na kuleta matokeo chanya kiutendaji yanayofanywa na kampuni hiyo kwa watanzania na Taifa kwa jumla.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kampuni hiyo, Tarehe 5 Januari, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Ameileza Bodi na Menejimenti kuwa wahakikishe TANOIL inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Malengo, Dhima na Azma ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo nchini.

Vilevile ameelekeza kuwa Viongozi hao watumie Mbinu zao, Taaluma na Uwezo Wao wote kuhakikisha kuwa Kampuni hiyo inatengeneza faida zaidi badala ya hasara kwa taifa na pia waepuke kuzalisha madeni.

Aidha ameelekeza TANOIL kushirikiana na TPDC, Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA) katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa yanashabihiana ili kuleta matokeo chanya ya kampuni hiyo katika kujiendesha.