Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

​MITAA ISIYO NA UMEME HANDENI...

​MITAA ISIYO NA UMEME HANDENI KUPATA HUDUMA HIYO IFIKAPO DESEMBA 2022

MITAA ISIYO NA UMEME HANDENI KUPATA HUDUMA HIYO IFIKAPO DESEMBA 2022

Imeelezwa kuwa, Mitaa 28 ambayo bado haina umeme katika Jimbo la Handeni mjini ipo katika mpango wa kupatiwa umeme kupitia mradi wa umeme vijijini Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Handeni Mjini, Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa ambaye aliuliza kuhusu mpango wa Serikali wa kupeleka umeme katika mitaa 28 ya Jimbo la Handeni Mjini ambayo bado haijapata umeme.

Naibu Waziri alisema kuwa, mitaa hiyo inapelekewa umeme na mkandarasi kampuni ya DERM ELECTRICS TANZANIA ambae yupo katika eneo la kazi na anaendelea na ujenzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Handeni.

Naibu Waziri aliongeza kuwa, Jimbo la Handeni Mjini lina jumla ya mitaa 60 ambapo kati ya mitaa hiyo, 32 ina umeme sawa na asilimia 53.3 na mitaa 28 haina umeme sawa asilimia 46.7.

Alisema kuwa kazi ya kupeleka umeme kwenye mitaa hiyo itakamilika Mwezi Desemba, 2022.