MLETE MWANAO BANDA LA WIZARA YA NISHATI.
Watoto ni viongozi wa kesho, na kujenga uelewa wao kuhusu masuala ya nishati kunaanza leo.
Mlete mwanao atembelee Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo atapata elimu kwa njia rahisi, ya kuvutia na yenye kufundisha kuhusu sekta ya nishati.
Na si elimu tu! Kila mtoto atapata zawadi maalum itakayomkumbusha yale aliyojifunza na kumhamasisha kuwa Balozi mzuri wa masuala ya nishati katika familia, shule na jamii.
Karibu Banda la Wizara ya Nishati, lililopo karibu na jengo la TANESCO, Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Tunawasubiri watoto na wazazi wao!