The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

MRADI WA EACOP WAFIKIA HATUA N...

MRADI WA EACOP WAFIKIA HATUA NZURI; SHEHENA YA KWANZA YATARAJIWA KUSAFIRISHWA JULAI 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umefikia hatua nzuri, ambapo ifikapo mwezi Julai mwaka huu, shehena ya kwanza ya mafuta inatarajiwa kuanza kusafirishwa kupitia Bandari ya Chongoleani, mkoani Tanga.

Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 7, 2026, mara baada ya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mazungumzo hayo, walijadili pia kuhusu mipango ya ujenzi wa mabomba mengine mawili ya kimkakati, ikiwemo bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda, pamoja na bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Uganda hadi Tanzania kabla ya kusafirishwa kwenda kwenye masoko ya nje.

Amesema ujenzi wa mabomba hayo mapya unatarajiwa kufanyika katika ushoroba wa bomba la EACOP.