Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula, ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula, leo Februari 04, 2026 amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa kinara wa kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia nchini.
Mhe. Chaula amesema kuwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma utaendelea kuunga mkono juhudi zote na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi. Aidha, ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuleta na kutekeleza mradi huo muhimu katika jiji la Dodoma.
Pia, amewapongeza wananchi wa Kikombo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na kuomba Serikali iendelee kuwaletea miradi ya maendeleo. Vilevile, amelishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta shule ya wasichana, akieleza kuwa ni hatua muhimu katika kuendeleza elimu kwa watoto wa kike.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Nishati Safi ya Kupikia katika Shule ya Sekondari ya Bunge iliyopo jijini Dodoma.