The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

Mwenyekiti aimiza Uadilifu nd...

Mwenyekiti aimiza Uadilifu ndani Wizara ya Nishati na Taasis zake

Mwenyekiti wa Kamati za Uadilifu ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake ambaye ni Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Innocent Luoga amefungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Wizara ya Nishati na Taasis zake, kilichofanyika Februari 03, 2026 mkoani Morogoro.

Kikao hicho kilichoandaliwa na Wizara ya Nishati kililenga kuimarisha uwajibikaji na maadili sehemu za kazi, kupata uelewa wa masuala ya kiutumishi pamoja na kubadilishana uzoefu ili kuongeza ufanisi Kazini.

Taasisi za Wizara ya Nishati zilizoshiriki kikao hicho ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).