Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Ministry of Energy

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWAS...

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWASILI RASMI OFISINI

Apokelewa na Katibu Mkuu na Wafanyakazi wa Wizara

Aahidi kushirikiana na wadau kumsaidia Mhe. Rais kufikia malengo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba, jijini Dodoma alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha. Felchesmi Mramba, Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dkt. Mataragio amesema, ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi na Taifa kwa ujumla.

"Mimi nashukuru kwa kuteuliwa kutumika katika nafasi hii, na nitaendeleza ushirikiano na watumishi wenzangu, ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake." Amesema Dkt. Mataragio.