Ni SIKU YA NANE SABASABA: WIZARA YA NISHATI TUPO HAPA KUKUHUDUMIA.
Ikiwa ni siku ya nane ya Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Wizara ya Nishati inaendelea kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lake katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika banda hilo, wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, gesi asilia, umeme, nishati jadidifu pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta ya nishati.
Wataalam wa Wizara na taasisi zake pia wanajibu maswali na kushughulikia changamoto pale zinapowasilishwa.
Karibu Sabasaba, karibu Banda la Wizara ya Nishati