The United Republic of Tanzania
Ministry of Energy

RANDAMA KUHUSU MAKADIRIO YA MA...

RANDAMA KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI WIZARA YA NISHATI 2026/2027 YAPITISHWA NA KAMATI YA BUNGE.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Subira Mgalu, leo imepitisha randama kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Randama hiyo imepitishwa baada Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi kuiwasilisha kwa kamati hiyo leo jijini Dodoma na baadaye kujadiliwa na Wajumbe wa kamati husika.

Pamoja na kuainisha mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027, randama imeainisha pia vipaumbele vya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2026/2027.

Kupitishwa kwa randama hiyo kunatoa fursa kwa Wizara ya Nishati kuandaa Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kuwasilisha katika Bunge la Bajeti.

Kikao cha kujadili randama kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Mafuta na Gesi Asilia), Dkt. James Mataragio pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara.