Shule 43 Ruvuma Zatumia Nishati Safi ya Kupikia kwa Ushirikiano na Wadau
Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika shule za sekondari 43 kati ya 153 zilizopo mkoani humo kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali.
Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Mwl. Edith Mpinzile, amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za pamoja kati ya viongozi wa shule, wazazi na wadau waliowezesha ujenzi wa majiko ya kisasa yanayokidhi matumizi ya nishati safi.
Ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi yanasaidia kulinda afya, kuhifadhi mazingira na pia kupunguza gharama za uendeshaji wa shule.
Aidha, Mwl. Mpinzile ametoa rai kwa wazazi na wadau kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili shule nyingi zaidi ziweze kunufaika na teknolojia hiyo.